DJ Choka
"Maisha ni kuendelea hadi zamu yangu ya kushinda ifike. Sikatishwi tamaa na kushindwa ndipo nitaona kuwa ugumu nikipindi cha mapito kuelekea mafanikio"
Kachumbari C: Jina lako la ukweli ni lipi?
DJ Choka: Hugoline Martin Mtambachuo
Kachumbari C: Nini kilichokufanya uwe DJ?
wasanii so na me nikapenda kuwa dj wa wasanii na kuwa tofauti na dj wa harusi au dj wa
radio
Kachumbari C: Ni vizingiti gani vikuu unavyokumbwa navyo kwenye u-DJ?
DJ Choka: Viko vingi unaweza kwenda sehemu na msanii ukakuta waandaaji wameandaa mashine
mbaya mbovu inabagua cd halafu kinachofuata ni kuaribu show ya msanii uliyekwenda nae
halafu mashabiki wanakuwa hawakuelewi wanajua ni mimi nimefanya makusudi.
Kachumbari C: Unadhani nini kifanyike ili kukuza na kuifaidisha sanaa ya muziki Tanzania?
DJ Choka: Kinachotakiwa kifanyike ni sisi wananchi kupenda sanaa ya nyumbani na kununua kazi za
wasanii wanaposikia album ya msanii imetoka na kuacha ulimbukeni wa kuchoma nyimbo
kwenye vibanda
Kachumbari C: Ni wasanii gani wa Bongo unaowakubali?
DJ Choka? Wako wengi sana ila kuna wale ambao mara kwa mara nakuwa nao na nafanya nao kazi
kama wakinichukua, kuna kaka yangu Prof Jay, AY, Mwana FA, Joh Makini, Jay Moe,
Roma, Fid Q, Mo Racka, Quick Racka, JCB, Nako 2 Nako nk
DJ Choka akiwa na kaka yake Prof. Jay
Mwana FA
AY akiwa na Romeo
Kachumbari C: Ni wasanii gani wa nchi za nje unaowakubali?
DJ Choka: Busta, Rick Ross, Ludacris, Eminem, Dj Khalid, Lil Wayne, Nick Minaj, 50 Cent, nk
Busta Rhymes
Nicki Minaj
Kachumbari C: Unadhani msanii gani chipukizi atakuja kung'aa sana hapo mbeleni?
DJ Choka: Mimi nadhani Dogo Janja na Dogo Asley kutoka TMK Wanaume Family
Dogo Asley
Dogo Janja
Kachumbari C: Kwa mtazamo wako,ili msanii aweze kung'aa katika sanaa ya muziki Bongo,awe na
vitu gani?
DJ Choka: Awe msafi tu..avae vitu vizuri kulingana na kazi yake anayoifanya, na kila siku atunge
nyimbo nzuri zitakazokubalika na jamii
Kachumbari C: Wasanii gani wa Bongo Movies unaowakubali?
DJ Choka: Kanumba, JB, Ray, Yusuph Mlela, Mdogo wangu Lulu, Jack Wolper, Aunt Ezekiel
Kanumba
Jacqueline Wolper
Ray akiwa na Mh.Jakaya M. Kikwete
Kachumbari C: Mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako mwaka 2012?
DJ Choka: Wategemee vitu vizuri tu, mimi sipendi kuahidi vitu halafu nisitimize so tunaomba pumzi tu
na nguvu ili malengo yatimie. ONE
Tidak ada komentar:
Posting Komentar